Upasuaji wa mwili wa mwanahabari raia wa Pakistani, Arshad Sharrif aliyeuliwa nchini Kenya umefanywa kubainisha jinsi alivyoaga dunia.
Mwanahabari huyo anasemekana kuuliwa kimakosa na maafisa wa polisi katika barabara ya Magadi- Kajiado akidhaniwa kuwa mshukiwa wa uhalifu aliyekuwa akisakwa.