Dukuduku kutokea mianya ya afisi za Mkuu wa idara ya ujasusi nchini George Kinoti na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji zawatia kiwewe miongoni mwa wakaribu wa mameneja wa halmashauri ya bandari nchini (KPA) kwamba lile shoka lililopura Waziri Henry Rotich na mkungo wake wa maafisa wa wizara, huenda likiwaangukia.
Kulingana na habari za ndani, ishara ipo kwamba wengi wao waliopo nyadhifani na wale waliostaafu hivi karibuni kamwe hawana budi ila kutia maji vichwa vyao kwani huenda wakanyolewa kisheria kufuatia mgorogo uliozushwa na tafaruku ya kampuni ya kitaifa ya sheheza za melini, KNSL ambayo yadaiwa kupigwa vita vya ndani kwa ndani kuanzia hapo.