×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands of Readers
★★★★ - on Play Store
Download Now

Ni muhimu kujenga undugu kanda ya Afrika Mashariki

Majuzi Rais Uhuru Kenyatta aliafanya ziara ya kibinafsi nyumbani kwa Rais John Pombe Magufuli mkoani Geita. Magufuli katika hotuba fupi ya kumkaribisha mwenzake alichekesha wengi aliposema kuwa alidhani kaja kumpa pole baada ya Harambee Stars kuifunga Taifa Stars 3-2 kule Misri katika michuono inayoendelea ya AFCON. “Nilipata simu ya Rais Uhuru akitaka kuja kunitembelea na nikakubali. Nilidhani kataka kunipa pole kwa Kenya kutufunga na hali tulikubaliana tuende sare 2-2. Hata hivyo nimemsamehe kwani walichapwa na Seneagl 3-0 na hali sisi tulifungwa na hao Senegal 2-0,” alitania Magufuli. Ziara ya Rais Uhuru ina umuhimu mkubwa hususan kukuza mahusiano ya nchi hizi mbili ambayo yalikuwa na uhusiano legelege.

Yamkini  matamshi ya mbunge fulani wa Kenya (jina twabana kwa ajili ya sheria) ya kuchochea kufukuzwa kwa wafanyibiashara watanzania Kenya kulilazimu Rais Uhuru kwenda haraka kutuliza hali ya uhasama iliyokuwa ikitokota. ‘Mwanasiasa huyo mwenye matamshi ya chuki si mwema na ni hatari kwa usalaam na amani’ asema Magufuli na kumshukuru Rais Uhuru kwa kuchukuwa hatua ya dharura kukarabati ufa huo ambao ulielekea kuanguka. Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa jadi kwani wakazi hapa huishi kindugu.Kuna makabila kama matano amabayo yako katika nchi hizi mbili. Makabila hayo ni Wamaasai, wakuria, wajaluo, waswahili na wadigo.

Get Full Access for Ksh299/Week
Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in