Kungamano ililosimamiwa na rais Obama pamoja na marais kutoka Kenya, Uganda na Ethiopia na mawakilishi wa Riak Machar na Salva Kir ni nafasi ya mwisho kupata suluhu kwa janga na maafa ya vita vilivyoikumba taifa la Sudan Kusini. Bwana Obama amedhihirisha bayana kwamba kama mazungumuzo hayatapata mafanikio, basi hakutakuwa na njia nyingine isipokuwa kuwawekea mahasimu hao vikwazo vya kiuchumi.
Mbarika ya Sudan Kusini ni donda ngumu kuponya. Kunayo changamoto tofauti zinazoungana pamoja kuzorotesha hali ya usalama huko. Jambo la kwanza ni kutapakaa kote Sudan Kusini kwa silaha ndogo kwa ajili ya miaka mingi ya vita nchini humo. Itabidi jamii ya kimataifa ipate njia ya kuzuia uagizaji wa silaha nchini humo.