Matarajio ya wengi kwamba Rais Uhuru Kenyatta angelegeza masharti ya Kudhibiti Maambukizi ya Korona kwa lengo la kufufua uchumi wa taifa, yamepata pigo baada ya masharti hayo kuongezwa.
Tukianza na mafuku ya kusafiri kwenye kaunti mbalimbali - Marufuku ya kuingia na kutoka kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera yameongezwa kwa siku nyingine thelathini huku Kilifi na Kwale zikifunguliwa kuanzia kesho saa kumi alfajiri.