Watu wengine 147 wathibitishwa kuambukziwa virusi vya korona nchini.

Kenya imeendelea kurekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya korona, leo hii watu mia moja arubaini na saba wakithibitishwa kuambukziwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema idadi hii kubwa mechangiwa na idadi kubwa ya sampuli zinazopimwa kwa muda uo huo. Mia moja arubaini na saba hao ni miongoni mwa watu elfu mbili mia anane thelathini na tisa waliopimwa hivyo kufikisha elfu moja mia sita kumi na nane idadi jumla ya maambukizi nchini. 

Nairobi imeendelea kuongoza kwa idadi ya maambukizi ambapo leo hii visa tisini vimethibitishwa Nairobi huku Mombasa ikirekodi visa arubaini na kimoja. Aidha idadi ya Kaunti ambazo zimeathirika zimefikia thelathini na mbili baada ya ile ya Nyeri na Uasin Gishu kurekodi maambukizi ya korona.

Aidha watu wengine kumi na watatu wamethibitishwa kupona na kufikisha ajumla ya waliopona nchini kuwa mia nne ishirini na mmoja. Hata hivyo, wagonjwa engine watatu wa COVID-19 wamefariki dunia wawili jijini Mombasa na mmoja kwenye kaunti ya Kiambu.

Wakati uo huo, wahudumu wa afya walioambukziwa virusi vya korona nchini ni hamsini na wanne. Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu wa Wizara katika Wizara ya Afya, Daktari Patrick Amoth aidha amesema hakuna mhudumu wa afya aliyefariki kutokana na virusi hivyo.