Mtu mmoja ameuliwa huku kadhaa wakilazwa katika Kaunti za Narok na Nakuru baada ya kujeruhiwa vibaya kufuatia makabiliano makali baina ya wakazi na wezi wa mifugo.
Katika Kaunti ya Nakuru mwanamume mmoja amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nakuru baada ya kufumwa mshale ambao umekwama mgongoni huku wengine watatu wakilazwa katika Hospitali ya Olenguruone wakiwa na majeraha mbalimbali. Wanne hao wamejeruhiwa katika makamiliano ya kikabila katika eneo la Olposimoru.