Kinara wa ODM, Raila Odinga ametoa ujumbe wa kuwapa motisha wachezaji wa timu ya taifa ya Harambe Stars, baada ya kupoteza mechi yao ya ufunguzi kwenye michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani afrika, AFCON dhidi ya Algeria.
Raila amewatambelea wanasoka hao kwenye kambi yao nchini Misri akiandamana na Mawaziri Amina Mohamed wa Michezo, Katibu Kirimi Kaberia na Balozi wa Kenya inchin Misri Joff Otieno.