Wapenzi wa jinsia moja wapata pigo

Hisia mbali mbali zinazidi kutolewa katika mitandao ya kijamii kufauatia auamauazi wa Mahakama Kuu wa kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa kupinga sheria za Kenya kuharamisha uhusiano wa jinsia moja. Uamuzi huo umetolewa na Majaji Chacha Mwita, Roselyne Aburili na John Mativo.

Kufuatia uamuzi huo baadhi yao wakilalamika kuwa haki zao zimekandamizwa huku wengi wakiwa na mafadhaiko kufuatia ubaguzi na kunyanyaswa.

Kundi la kutetea haki zao liliwasilisha kesi hiyo kwa kusema katiba ya Kenya imeweka wazi kuwa watu wote ni sawa kwa kigezo cha sheria. Hata hivyo, mahakama imetoa uamuzi kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kwamba wamekuwa wakinyanyaswa.

Mashirika matatu ya kupigania haki za jisia moja mwaka wa 2016 yaliwasilisha keshi ya kutaka sehemu za 162 (a) na 165 ya Penal Code zinazoharamisha mahusiano ya jinsia moja kutajwa kuwa zilizo kinyume na sheria, yakisema zinachangia kubaguliwa kwao, kunyimwa haki ya kujieleza, haki ya kupata matibabu na kuheshimiwa sawa binadamu wengine.

Katika uamuzi wao, majaji Chacha Mwita, Roselyne Aburili na John Mativo wamesema kuwa kaida za kijamii na utamaduni ni sharti ziheshimiwe na kwamba kuruhusu mahusiano ya jinsia moja kutachagia ndoa za aina hiyo.

Uhusiano wa jinsia moja umepigwa marufuku nchini tangu karne ya 19 na yeyote atakayepatikana na kosa hilo akihukumiwa kifungo cha kumi na minne.

Kulingana na utafiti, uhusiano wa jinsia moja unaaminika kuanzia katika taifa la Ugiriki, Uchina, Japani. Barani Afrika, uhusiano huo unaamika kuanzia taifa la Misri.

Hata hivyo, dini zote zinapinga uhusiani wa aina hiyo huku katika Bibilia kitabu cha Mambo ya Walawi kikisema; "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo kwa Mungu". Katika Quran Sura  aa'raf ama sura ya saba aya ya themanini, Hakika ninyi mnafika kwa wanaume kwa kuwaingilia badala ya wanawake, bali ninyi ni watu warukao mipaka.

Baadhi ya marais wa Afrika wamepinga waziwazi uhusiano wajinsia moja. Rais Obama alipokuwa Kenya 2015, Rais Kenyatta aliweka wazi kuwa hilo si suala muhimu kwa Wakenya, kauli aliyorejelea mwaka jana alipohojiwa katika runinga ya CNN.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipitisha mswada wa kupinga uhusiano huo akisema kuwa yeyote atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria. Akihojiwa na Runinga ya CNN mwaka wa 2016 Museveni alitoa wito kwa mataifa ya ughaibuni kuheshimu mila na tamaduni za Waafrika.

Katika mtandao wa Twitter hisia mbalimbali zimetolewa kutumia alama ya reli #Repeal162  Makundi hayo yanaitaka mahakama kuagiza sehemu ya 162 ya sheria za Kenya kufanyiwa marekebisho.

Uamuzi huo unajiri siku chache baada ya Mshindi wa tuzo kadhaa za uandishi na mtetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja Binyavanga Wainaina kufariki dunia.

Related Topics