Seneta wa Kakamega, Cleophas Malala amepinga vikali kuhusika katika mauaji ya Matungu na kuhusishwa na aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa akisisitiza kuwa yeye na Echesa hawajonana kwa muda kufuatia tofauti zao za kisiasa.
Akizungumza wakati wa mahojiano na kipindi cha Maisha Asubuhi na Leo hii, Malala amedai kuwa kukamatwa kwake ni njia ya kufunika uhalifu wenyewe.