Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema zote kubwa na ndogo.Asalam aleikum warahmatullahi taala wabarakatu.Saum Kareem..saum maqbul! Tukiwa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan hatuna budi kutowa shukurani zetu kwa Allah Jallah Jallallu kutuwezesha kuona siku ya leo. Ni wengi walioazimia kuwa katika funga hii ya saumu iliyo na faida sufufu lakini hawakuweza kwani wameenda mbele ya haki.
Mimi na wewe tuna bahati kuwa twapumuwa hewa ya Allah Azzah Wajallah kupata fursa hii adimu kuweza kuvuna mengi yaliyo katika mwezi huu unaokuja mara moja kwa mwaka. Funga ama saumu hii ya mwezi wa Ramadhani imezungukwa na neema za kila aina. Neema hizi ziko katika nukta za kijamii, kiroho, kiuchumi na kimaadili na pia kiafya.