Gavana wa Meru ateteta matumizi ya fedha mbele ya seneti

Gavana wa Meru, Kiraitu Murungi amefika mbele ya Kamati ya Uhasibu wa Fedha katika Bunge la Seneti, ili kueleza kuhusu matumizi ya fedha katika serikali yake kufuatia Ripoti ya Mkaguzi wa Bajeti kwenye mwaka wa kifedha 2017/2018.

Miongoni mwa maswali aliyofaa kujibu ni likiwamo lile la rekodi za matumizi ya fedha katika Mfumo wa IFMIS, ambapo ilibainika kuwa dosari zilizokuwapo zilisababishwa na ukosefu wa ufahamu wa maafisa wa serikali ya Meru kuhusu jinsi ya kuhifadhi taarifa hizo katika mfumo huo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moses Kajwang amemtaka Gavana Murungi kuihakikishia kamati hiyo kwamba, atafanikisha mafunzo kwa maafisa wake ili kuepusha dosari hizo siku zijazo.

Akizungumza kwa niaba ya gavana, Waziri wa Fedha katika kaunti ya Meru, Kabii Chabari amesema tayari maafisa waliozembea kazini walifutwa kazi. 

Related Topics