Standard yazindua jarida kuhusu masuala ya Ramadhan

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Shirika la Habari la Standard limezindua jarida litakaloangazia masuala kuhusu umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Jarida hilo linawalenga hasa waumuni wa dini ya Kiislamu msimu huu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Standard Group Orlando Lyomu amesema lengo ni kuwafikia wateja wote mbali na kuwafunza wengine kuelewa kuhudu dini ya Kiislamu.

Wakati uo huo, ametangaza kuwa sehemu ya fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya jarida hilo zitatumika kutoa misaada kwa wasiojiweza katika jamii.

Aidha amesisitza kwamba shirika hilo litaendelea kuangazia masuala yanayolenga kuinufaisha jamii kwa jumla. Viongozi wa Kiislamu ambao wamhudhuria hafla hiyo wamesema kuna haja ya waumini kujitolea kutoa mafunzo yanayofaa kwa jamii. Yisuf Nzibo ni Katibu Mkuu wa Baraza la wahubiri wa Kiislamu SUPKEM.

Mwanahabari wa Radio Maisha Ali Hassan amesema ushirikiano huo utakuwa wa manufaa kwa waumini wa Kiislamu.

Jarida hilo litakuwa likitolewa kila mwaka wakati wa Ramadhan.

For More of This and Other Stories, Grab Your Copy of the Standard Newspaper.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

Ramadhan