Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks,Julian Assange amehukumiwa wiki 50 kwa kosa la udukuzi Uingereza

Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange anayehusishwa na udukuzi amehukumiwa wiki  50 jela na mahakama moja ya Uingereza. Akitoa uamuzi huo, Jaji Deborah Taylor amesema Assange alitumia mamlaka yake kukiuka sheria na kuudharau mfumo wa mahakama wa taifa hilo. 

Assange alishtakiwa kwa kukiuka sheria za kuachiliwa kwa dhamana na kutafuta hifadhi kwa kipindi cha miaka 7  katika Ubalozi wa London kufuatia madai ya dhulma za kingono nchini  Uswidi.

Alishtakiwa na wanawake wawili wa Uswidi ambao walidai kwamba aliwadhulumu kingoni mwaka 2010 kukiwamo kuwabaka. Hata hivyo Assange alikana mashtaka dhidi yake.

Ikumbukwe mtaalam huyo wa masuala ya mitandao kwa wakati mmoja alishtumiwa kwa kudukua siri za taifa la Marekani.