Wafanyakazi nchini watalazimika kusubiri kwa muda zaidi kabla ya kujua iwapo wataongezewa mishahara au la. Ilitarajiwa kwamba huenda serikali ingetengaza nyongeza hiyo wakati wa maadhimisho ya Leba Dei. Hata hivyo, Waziri wa Leba Ukur Yattani aliyemwakilisha Rais Uhuru Kenyatta, amesema mazungumzo yatafanyika wiki hii baina ya serikali na washikadau mbalimbali kuhusu suala hilo suala ambalo limewaghadhabisha wafanyakazi.
Akihutubu wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi, Waziri wa Leba Ukur Yattani amesema mazungumzo hayo ndiyo yatakayobaini iwapo wafanyakazi wataongezwa mishahara au la.