Swazuri kusalia rumande hadi tarehe 2, Mei

?

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi Mohammed Swazuri atasalia rumande hadi tarehe 2 mwezi Mei wakati ambapo Jaji Mumbi Ngugi ataamua iwapo ombi lake la kupunguziwa dhamana ya ksh 12M litakubwaliwa au la.

Swazuri amerejea mahakamani mapema leo kusikiliza uamuzi kuhusu ombi alilowasilisha akiitakaa Mahakama ya Kukabili Ufisadi ipunguze kiwango cha dhamana ilichomwagiza alipe kabla ya kuachiliwa huru.

Jumatano, Jaji wa Mahakama Kuu, Mumbi Ngugi alilitaja  kuwa la dharura ombi hilo na kumwagiza Swazuri kuwasilisha waraka wa ombi la kupunguzwa kwa dhamana yake kwa Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP.

Mahakama hiyo ilimtaka alipe dhamana ya shilingi milioni 21 pesa taslimu ama bondi ya shilingi elfu 30. Hata hivyo, Swazuri aliutaja uamuzi huo wa Hakimu Mkuu, Lawrence Mugambi kuwa unaokiuka katiba kwa kumtoza kiwango cha juu.

 Swazuri pamoja na washukiwa wengine 10 walitaka kuwachiliwa huru, baada ya kukaa korokorini kipindi chote cha sherehe za Pasaka wakisubiri uamuzi kuhusu ombi la kuachiliwa kwa dhamana.

Washtakiwa hao ni aliyekuwa Kamishna wa NLC, Emma Njogu, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo, Tom Aziz Chavangi, Salome Munubi na Katibu wa tume hiyo, Lilian Kaverenge. Wengine ni Francis Mugo, Samuel Rugongo, Godfrey Muritu, Evamary Wachera, Michael Oloo na Catherine Wanjiru. 

Related Topics

Mate tongola