Zaidi ya watu 100 wamefariki dunia kufuatia shambulio la kigaidi, Siri Lanka

Zaidi ya watu mia moja wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Sri Lanka kufuatia mashambilio katika makanisha matatu na hoteli mbili mapema leo wakati wa maadhimisho ya Jumapili ya Pasaka.

Mashambulio hayo yametekelezwa katika mji Mkuu Colombo na mengine mawili eneo la Negombo Mshariki mwa mji wa Batticaloa.

Kulingana na maafisa wa usalama  wengi waliofariki na waliojeruhiwa ni waumini waliokuwa makanisani na  wageni waliokuwa kwenye hoteli zilizoshambuliwa. Aidha inaaminika walioyatekeleza mashambulio hayo walikuwa walipuaji wa kujitolea muhanga.