Mhudumu wa bodaboda amefariki dunia kufuatia ajali Barabara Kuu ya Makindu- Wote

Mhudumu mmoja wa bodaboda amefariki dunia kwenye ajali ya barabarani kwenye Barabara ya Makindu- Wote.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwanamume huyo,  Shadrack Kilonzo mwenye umri wa miaka 30 alipoteza udhibiti wa pikipiki yake alipokuwa akitoka katika sherehe ya familia hali iliyomfanya kuanguka na kujeruhiwa kichwani hali iliyosababisha kifo chake alipokuwa akipelekwa hospitalini.

Mwili umepelekwa katika Hifadhi ya Makueni ukisubiri kufanyiwa upasuaji.