Madaktari wawili wa Cuba ambao wamekuwa wakihudumu kwenye Kaunti ya Lamu , wahama kwa kuhofia usalama wao

Madaktari wawili wa  Cuba  ambao wamekuwa wakihudumu kwenye  Kaunti ya  Lamu tangu mwezi Julai mwaka jana, wamehama wakihofia usalama wao, siku chache tu baada ya wenzao wawili kutekwa nyara Mjini Mandera . Imethibitishwa kwamba wawili hao wameondoka kwenye Kaunti hiyo wekendi hii.

Kamishana wa Lamu Joseph Kanyiri,  amepuuzilia mbali suala hilo akisema wawili hao wameitwa Jijini Nairobi kuhusu maswala ya kazi  yao.  Aidha amedokeza kwamba Lamu ni salama ikilinganishwa na Mandera.

Waziri wa afya kwenye Kaunti la Lamu Anne Gathoni, amethibitisha kwamba madaktari hao wamehama sehemu hiyo, lakini amekanusha madai kwamba kuondoka kwao hakuhusiani na swala la ukosefu wa  usalama.

Tangu kutekwa nyara kwa madaktari wawili wa Cuba siku ya Ijumaa na kundi  Al Shabab ,  madaktari wengine waliokuwa wakihudumu kwenye Miji za  Wajir na Garissa wamelazimika kurejea Nairobi.

Related Topics