Zaidi ya watu 200 kwenye Kijiji cha Sesia, Kaunti ya Samburu wanaendelea kutibiwa baada ya kula mzoga wa ngamia aliyekufa baada ya kuugua

Zaidi ya watu 200 kwenye Kijiji cha Sesia, Kaunti ya Samburu wanaendelea kutibiwa baada ya kula mzoga wa ngamia aliyekufa baada ya kuugua.

Kundi la maafisa wa afya wakiongozwa na Afisa wa Idara ya afya kwenye kaunti Daniel Lomukuny limejenga kitua cha muda cha kuwashughulikia walioathirika.

Amesema kufikia sasa jumla ya watu mia mbili hamsini na wanane wametibiwa na hali yao imeimarika. Aidha amesema wegi walioathirika ni kina mama na watoto, huku akisema ngamia aliyekufa amekuwa akitibiwa kwa siku kadhaa.

Mbunge wa Samburu Mashariki Jackson Lekumontare amesema wakazi walioathirika walilazimika kula mzoga huo kutokana na makali ya njaa, kwani Kuanti ya Samburu ni miongoni mwa zilizoathirika na kiangazi.