Mshukiwa Mkuu, Erick Adede anadaiwa kuwa mmliki wa kasha hilo lililokuwa na shilingi bilioni 2 pesa bandia

Mahakama imemwachilia kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu mshukiwa mkuu anayehusishwa na kasha la fedha bandia zilizopatikana katika Benki ya Barclays Tawi la Queens Way siku chache zilizopita. Washukiwa wengine watatu wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja.

Mshukiwa Mkuu, Erick Adede anadaiwa kuwa mmliki wa kasha hilo lililokuwa na shilingi bilioni 2 pesa bandia. Washukiwa wengine ni Ahmed Shah aliyejidai kuwa mwekezaji wa kimataifa, Elizabeth Muthoni na Irene Wairimu Kimani.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

Money launderingErick Adede