Wakuu wa KNUT wamefika mbele ya kamati ya bunge ya elimu kuzungumzia uhamisho wa walimu

Wawakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT wamefika mbele ya Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa kuzungumzia mpango wa kuwahamisha walimu wakuu hadi kwenye maeneo mengine nchini ambao wameibua masuala kadhaa ambayo hayawaridhishi kuhusu mpango huo.
Miongoni mwa masuala haya ni kuwapa walimu wakuu uhamisho hadi kwenye maeneo ya mbali hali inayoibua changamoto kuu ya mawasiliano baina ya walimu hao na wakazi kutokana na tofauti za lugha. Clement Omollo ni Katibu Msaidzi a chama hicho
 
Hata hivyo mmoja wa wanakamati hiyo ya elimu amesema pingamizi zinazoibuliwa na walimu kuhusu uhamisho huenda zikawanyima fursa za kazi kwenye maeneo mengine ya nchi iwapo hawako tayari kwa uhamisho jambo ambalo limepingwa na maafisa wa KNUT.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo. Julius Melly amesema masuala  yaliyoibuliwa na walimu yatatathimiwa kwa kina na mapendekezo yao kuwasilishwa kwa mwajiri wao.
 
 

Related Topics