Msako wa vijana wanaowauwa wazee kwa dhana kwamba ni wachawi unaendelea

Mshirikishi wa Utawala eneo la Pwani John Elungata ameonya kukabiliwa kwa mujibu wa sheria vijana ambao wamekuwa wakiwauwa wazee kwa dhana kwamba ni wachawi.
 

Kulingana na Elungata suala hilo limekuwa likichochewa na masuala tofauti ukiwamo urithi wa mali ambayo yamekuwa yakimilikiwa na wazee.

Elungata amewahimiza wakazi wa Pwani kushirikiana na Idara ya Usalama katika vita dhidi ya suala hilo linaloendelea kukithiri.

Hayo yanajiri huku ikibainikwa kwamba zaidi ya wazee 60 kwenye Kaunti ya Kilifi pekee wameuliwa kufuatia shutuma hizo, Wadi ya Mwawesa iliyo eneo bunge la Rabai ikitajwa kuongoza kwenye visa hivyo.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman