Rais:Wakenya katika mataifa mengine washauriwa kuchukua pasipoti za kisasa kwenye mataifa hayo

Rais Uhuru Kenyatta amewaagiza Wakenya wanaoishi katika mataifa mengine kuhakikisha kuwa wanapewa pasipoti za kisasa kwenye mataifa hayo. Rais ambaye yuko ziarani nchini Namibia ametoa agizo hilo kwa idara ya Uhamiaji na Wizara ya Mashauri ya Nchi za nje, wakati alipokutana na wakenya wanaoishi nchini humo.

Rais amesema kuwa haina haja kwa Wakenya hao kusafiri hadi humu nchini kupata stakabadhi hiyo muhimu.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.