Dawa za serikali zapatikana zikiuzwa Transzoia

Polisi kwenye Kaunti ya Trans Nzoia wamefainiwa kuzinasa dawa za thamani isiyojulikana katika hospitali moja binafsi zinazodaiwa kuibwa kutoka katika hifadhi ya serikali ya kaunti.

Mkuu wa Polisi wa Kiminini, Stephen Tumbo ameongoza oparesheni katika Hospitali ya Kiminini Cottage na kufanikiwa kuyanasa masanduku 167 yaliyokuwa na dawa hizo zilizokuwa na nembo ya Hospitali ya Rufaa ya Kitale. Afisa mmoja wa cheo cha juu katika hospitali hiyo na dereva ni miongoni mwa waliokamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa dawa hizo.

 Afisa wa Upelelezi kwenye kaunti hiyo, Peter Kimalwa amesema maafisa kadhaa wa kaunti hiyo wamehojiwa kuhusu suala hilo huku uchuunguzi ukiendelea.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.