Mchakato wa kukusanya saini ili kuvunjwa kwa Bunge la Kaunti ya Mombasa unaendelea huku Mashirika ya Kijamii yakisema kwamba Gavana Joho hana mamlaka Kikatiba kulivunja bunge hilo.

Mchakato wa kukusanya saini ili kuvunjwa kwa Bunge la Kaunti ya Mombasa unaendelea huku Mashirika ya Kijamii yakisema kwamba Gavana Joho hana mamlaka Kikatiba kulivunja bunge hilo.

Kulingana na mashirika hayo, gavana Joho amekuwa akiwahujumu wawakilishi wadi hasa wanapoukosoa uongozi wake. Wawakilishi wadi hao wameshauriwa kuhakikisha wanaendesha shughuli zao bila kutishwa na yeyote.

Mwalimu Rama anayehudumu na mashirika hayo aidha amesema kwamba wawakilishi hao wana haki ya kuangazia jinsi fedha za kaunti zinavyotumika vilevile utendakazi wa mawaziri na gavana huyo.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Wakili Zedekiah Adika ambaye anasema serikali  ya Kaunti ya Mombasa  inanjama ya kuwakandamiza  wawakilishi hao ili ikwepe  majukumu yake.