Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa imewahoji washikadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhusu masuala muhimu ya sekta hiyo.

Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa imewahoji washikadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhusu masuala muhimu ya sekta hiyo. Miongoni mwa wale ambao wamefika mbele ya kamati hiyo ni Muungano wa Kitaifa wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili KESHA na Chama cha Kitaifa cha Wazazi.

 Kamati hiyo imejadili ripoti ya washikadau hao kuhusu mtalaa mpya wa elimu ambao umeanza kutekelezwa mwaka huu, kiwango cha fedha kinachotengewa shule za umma na serikali na mpango wa kuvisambaza vitabu vya kiada katika shule hizo za umma na mpango wa kuwahamisha walimu.

Wabunge wametaka kufahamu jinsi wanavyoshughulikia changamoto katika sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja anayesitisha masomo yake kutokana na sababu moja au nyingine. 

Related Topics

Kamati Elimu Bunge