Kamati maalum ya wataalam kuelekea nchini Cuba kuchunguza mazingira yaliyosababisha kifo cha daktari

Kamati maalum ya wataalam inaondoka nchini Jumatano usiku kuelekea nchini Cuba kuchunguza mazingira yaliyosababisha daktari mmoja miongoni mwa waliotumwa nchini humo kujiua.

Waziri wa Afya Sicily Kariuki amesema kamati hiyo maalum itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Rashid Aman, inatarajiwa kuwasilisha ripoti na mapendekezo yake baada ya siku tano.

Waziri Kauriuki amesema taraifa kuhusu kujiua kwa daktari hiyo zimeripotiwa tu katika vyombo vya habari na shrti uchunguzi wa kina ufanywe.

Daktari Hamisi Ali Juma anasemekana kujiua tarehe 17 Mwezi huu baada ya serikali kupuuza ombi lake kurejea nchini kuishughulikia familia yake. Hamisi ni miongoni mwa madaktari hamsini wlaiotumwa Cuba kufuatia mkataba baina ya serikali za mataifa haya mawili.

Kuna jumla ya madaktari mia moja wa Cuba walio nchini chini ya mkataba huo.