Balozi wa Zambia humu nchini Brenda Muntemba amefariki dunia

Balozi wa Zambia humu nchini Brenda Muntemba aliyehusika katika ajali eneo la Lukenya mwezi uliopita amefariki dunia.

Inaarifiwa Muntemba amefariki dunia akiendelea kutibiwa katika hospitali ya Nairobi katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Ikumbukwe ajali hiyo iliyotokea tarehe 26 mwezi jana ilihusisha gari la mwezake wa Botswana’s Duke Lephoko eneo al Lukenya kwenye barabara kuu Nairobi-Mombasa.

Walikuwa wakielekea Nairobi baada ya kuhudhuria mkutano eneo la Maanzoni, Athi River. Walilazwa katika hospitali ya Machakos Level Five kabla ya kuhamishiwa Niarobi Hospital

Related Topics

Brenda Muntemba