Prof George Magoha aidhinishwa rasmi na bunge kuwa waziri

Bunge limeidinisha  uteuzi wa Profesa George Magoha kuwa waziri mpya wa Elimu. Kiongozi wa wachache kwenye bunge la Kitaifa John Mbadi, amewasilisha ripoti na mapendekezo kuhusu uteuzi huo baada ya kumchuja Magoha juma lililopita.


Bunge sasa litajadili mapendekezo ya kamati hiyo kuhusu uteuzi wake kesho alasiri. Alipofika  mbele ya Kamati  ya Uteuzi  Magoha alisema anatajriba na uzoefu wa kutosha katika nyanja ya elimu ambapo amehudumu kwa muda mrefu.


Magoha amemtaridhi Amina Mohammed ambaye amehamishiwa Wizara ya Michezo ambayo awali ilishikiliwa na Rashid Echese aliyesimamishwa kazi na  Rais Uhuru Kenyatta. 

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman