Joho ajitetea mbele ya Kamati ya Seneti

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amejitetea mbele ya Kamati ya Seneti  iliyobuniwa kutatua   mzozo wa kisiasa kati yake na wawakilishi wadi wa Bunge la Mombasa. Mzozo huo uliibuka baada ya Joho kudaiwa kuwa na mpango wa kuwabandua wawakilishi wadi suala ambalo amelikana vikali.

Joho amejitetea vikali dhidi ya madai hayo amesema kilichopo kwa sasa ni mvutano baina ya Spika wa Bunge na baadhi ya maafisa katika serikali.

Spika Aharub Kahtr vilevile alikuwa amealiwa japo alituma arafa akieleza kwamba hangeweza kufika kwani anaugua.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Seneta wa Laikipia John Kinyua inatarajiwa kutanzua kiini cha mchakato ambao tayari umeanzishwa na vuguvugu la Oparesheni fagia bunge.

 Kulingana na katiba ya taifa kipengele cha 104, wapiga kura tu ndio wenye uwezo wa kumnga'atua mamlakani  mbunge  yeyote kabla ya kukamilika kwa muda wake uongozi.

Kadhalika inasema kwamba bunge litaanzisha shughuli ya kuchunguza madai yanayolengwa  kabla ya kutimuliwa kwa kiongozi yeyote. Gavana Joho amesema atazindua shughuli  ya kukusanya saini ya wakazi kuwatimua wawakilishi  hao uongozini.

Related Topics