Mhubiri James Ng'ang'a aendelea kuhojiwa katika Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi DCI

Mhubiri mwenye utata wa Kanisa la Neno Evangelism, James Ng'ang'a anahojiwa katika Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi DCI, baada ya kukamatwa usiku wa kuamkia leo kwa kumtishia maisha mwanahabari wa runinga ya Citizen Linus Kaikai.

Mhubiri huyo alikamatawa baada ya Kaikai kurekodi taarifa katika DCI kufuatia tisho la Ng'ang'a ambaye anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani baadaye leo.

Kiongozi huyo wa kidini alitoa vitisho hivyo kupitia kanda ya video iliyosambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii huku akijiita “Chief General Commander” na kutoa vitisho dhidi ya Kaikai bila ya kufafanua hatua ambazo angechukua.

Vitisho hivyo vilitolewa kufuatia kauli ya Kaikai kuwa ni wakati serikali iweze kuwadhibiti wahubiri nchini ambao anasema asilimia kubwa wamekuwa wakiwalaghai wananchi mamilioni ya pesa.

Related Topics