Wanafunzi kadhaa wa Shule ya Kitaifa ya Wasichana ya Nyabururu Kaunti ya Kisii wamelazwa katika hospitali mbalimbali baada ya kula chakula chenye sumu. Hata hivyo baadhi wametibiwa na kuruhusiwa kuondoka.
Baadhi ya wanafunzi ambao hawakutaka watajwe wamesema walionywa dhidi ya kuwaeleza wazazi wao, la si hivyo wangeadhibiwa wakati wangefika shuleni na kwamba shule ingegharamia matibabu yao.
Afisa mmoja wa afya wa hospitali ya Nyangena ambaye pia hakutaja kutajwa amesema jumla ya wanafunzi ishirini wametibiwa tangu walipowasilishwa Alhamisi. Amesema wamebaini kuwa waliokuwa wakiugua walikula chakula ambacho hakikuwa salama.