Marubani Argentina wakataa kupaa na Ndege aina ya Boeing 737-8 Max

Marubani nchini Argentina wamekataa kata kata kupaa na ndege aiana ya Boeing 737-8 Max kufuatia ajali iliyohusisha ndege ya iana hiyo nchini Ethiopia.

Licha ya taifa hilo kutotangaza  matumizi ya ndege hiyo, hatua hiyo  sasa italifanya Argentina kuwa miongoni mwa mataifa ambayo yanasubiri ripoti ya uchunguzi wa wa ajali ya ndege ya Ethiopia 302 kabla ya kuanza kupaa tena.

Mataifa engine ambayo yamesitisha safari hizo ni Brazil, China, Singapore, Indonesia, Afrika Kusini, Mexio na Ethiopia yenyewe.

Hata mataifa mengine hayajasitisha safari za ndege ya aian hiyo yakiwamo Oman Air, Flydubai  Russia s7 na Turkish Airline.

Nchini Marekani iliki kampuni ya Boeing, wasimamizi wa kampuni wametahadgrishwa kuwa tayari kufanya mageuzi kutokana na uchunguzi utakaofanywa.