Rais Uhuru Kenyatta leo anatarajiwa kufungua rasmi Kongamano la Ugatuzi liliong'oa nanga mapema jana katika Chuo Kikuu cha Kirinyaga.
Kongamano hilo linatarajiwa kuangazia hatua zilizopigwa na kaunti mbalimbali katika kuwainisha ajenda zake na ajenda nne kuu za serikali ya Jubilee kufuatia mjadala ulioanza katika Kongamano la Ugatuzi mwaka uliopita kwenye Kaunti ya Kakamega. Kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu kwa kiingereza ni Deliver, Transform, Measure, and Remain Accountable.