Afueni kwa wakulima wa miwa baada ya serikali kuweka mikakati ya kukabili changamoto

Huenda wakulima wa miwa katika sehemu mbali  nchini, wakapata afueni baada ya Serikali ya Kitaifa kuweka mikakati kwa ushirikiano na Viongozi mbalimbali ili kukabili changamoto zinazoikumba Sekta ya Sukari.

Katika kikao kilichoongozwa na Kinara wa ODM Raila Odinga, kwenye ofisi za Capital Hill, Odinga amesema kwamba viongozi wameafikiana kuwashirikisha washikadau wote kuimarisha kilimo cha miwa ili  kutatua masaibu ya wakulima.

Waziri wa Kilimo mwangi Kiunjuri kwa upande wake amesema kwamba Sekta ya Sukari inakumbwa na changamoto si haba ,akisema wakulima wanataabika kutokana na kunyanyaswa na viwanda vya kutengeneza sukari

Mkutano huo unajiri wakati ambapo sekta ya sukari inakabiliwa  na matatizo tele huku wakulima wa miwa kwenye maeneo mbalimbali wakizidai kampuni za sukari malimbikizi ya madeni yao. Aidha suala la ufisadi  kwenye usimamizi wa viwanda hivyo umetajwa kuwa kizingiti kwenye ukuaji wa kilicho cha miwa.

Related Topics