Tume ya IEBC yashauriwa kutatua mzozo wa Mipaka Baringo

Viongozi wa eneo la Baringo wakiongozwa na Gavana Stanely Kiptis na Mbunge wa Baringo Kusini Charles Kamuren wametoa wito kwa Tume ya Uchaguzi, IEBC kuharakisha tatizo la mpaka linatatuliwa kwenye kaunti hiyo.

Wamesema mzozo huo ndio unasababisha mivutano baina ya jamii mbalimbali hali ambayo imechangia watu kadhaa kuuliwa na wala sio wizi wa mifugo inavyoaminika.

Aidha wakazi wa eneo hilo wameilaumu serikali kuu kwa kutowachukulia hatua zozote viongozi wa kisiasa, ambao wanachochea ghasia licha ya kuwafahamu. Ssasa wamependekeza, jopo kazi maalum kubuniwa kutatua mzozo huo.

Viongozi hao walikuwa wakizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya watu watano waliouliwa siku cahche zilizopita na washukiwa wa wizi wa mifugo.

Ikumbukwe mvutano unajiri huku mpaka kwenye eneo la Mututani umekuwa ukiipua hisia huku baadhi ya viongozi wa Pokot wakidai eneo la Mukutani liko Tiaty.

Hali hii imesababisha kucahguliwa kwa machifu wawili mmoja anayewakilisha mukutani waliko watu wengi wa jamii ya Ilchamus na mwingine Makutano kuwawa Wapokot wa wadi ya Taglubei.