Polisi kwenye Kaunti ya Narok wanafanya uchunguzi kufuatia kisa ambapo mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu umepatikana katika chumba kimoja cha kukodi. Chifu wa eneo hilo, Titus Tonui amesema mwanafunzi huyo ametambuliwa kuwa wa Shule ya Upili ya Kisiara. Tonui amesema imebainika kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na huenda alifariki dunia alipokuwa akijaribu kuavya mimba.