Spika wa Bunge la Kaunti ya Tharaka Nithi, Susan Ngugi ameng'atuliwa mamlakani.

Naibu Spika wa Bunge la Kaunti ya Tharaka Nithi, Susan Ngugi ameng'atuliwa mamlakani huku wawakilishi wadi wakimshtumu kwa utumiaji mbaya wa mamlaka.

Aidha inaarifiwa Ngugi amekuwa akitumia lugha isiyoendana na wadhifa wake katika bunge hilo. Kisa cha kubanduliwa kwake kinajiri miezi michache tu baada ya Bunge la Nairobi kumtimua mamlakani Spika Beatrice Elachi.

Aidha Spika wa  Homa Bay Elizabeth Ayoo na Maurice Buluma wa Kakamega walitimuliwa mwaka uliopita.