KOT walihakikisha gazeti la New York Times linaomba radhi na kuondoa picha walizochapisha

Tangu kuzinduliwa kwa mitandao ya kijamii, mitandao hiyo imetumiwa kuwa njia ya kushirikiana, na hata kuleta mabadiliko. Katika mtandao wa Twitter, Wakenya wanao utumia mtandao huo maarufu KOT, Kenyans On Twitter, wamesifika sana kwa kuhakikisha sifa za taifa hili haziharibiwi vilevile kugakikisha mashujaa  wanapokea heshima wanayo stahili.

Wiki iliyopita Wakenya hao walihakikisha gazeti la New York Times linaomba radhi na kuondoa picha walizochapisha za watu walioaga dunia wakati wa shambulio katika hoteli ya DUSIT D2  bila kuficha sura zao.

Alama ya Reli iliyotumiwa ni #SomeOneTellNewYorkTimes na #DeportKimiko, Kimiko akiwa mwandishi wa NewYork Times aliyeandika taarifa hiyo. Vilevile Kimiko anatarajiwa kuwa Mkuu wa gazeti hilo kwenye la Afrika Mashariki.

Vilevile wiki iliyopita, Mwanariadha,Eliud Kipchoge aliteuliwa miongoni wanaspoti maarufu wakiwamo LeBron James, Lewis Hamilton, Kylian Mbappe katika tuzo ya Laureus World Sportsman Of The Year. Lakini kilicho waghadhabisha Wakenya ni  picha ya Kipchoge iliyotumiwa na Laureus miongoni mwa wawaniaji wengine. Picha hiyo ilipigwa wakati Kipchoge alikuwa uwanjani akikimbia huku kamasi likimtoka hali ilioyoilazimu Laureus kusalimu amri na kubadili picha hiyo.

Aidha, mwaka wa 2015 kabla ya ziara ya aliyekuwa  Rais wa Marekani ,Barrack Obama nchini, Wakenya katika Mtandao wa Kwitter walikishambulia Kituo cha Habari cha CNN na alama ya Reli #SomeOneTellCNN baada ya CNN kusema kuwa  Obama anazuru taifa lilokuwa na mashambulio mengi ya kigaidi  yaani a hot bed of terror.

Mwaka wa 2013 Askofu wa Marekani TD Jakes aliolazimika kuwaomba msamaha Wakenya baada ya kusema kuwa Wakenya wote wanakunywa maji safi kwa sababu ya kanisa lake ,na hospitali nchini Kenya zimeimarika kwasababu ya Kanisa lake. 

Mchungaji mwingine naye wa Marekani kwa jina Pat Robertson pia alipata dozi ya Wakenya mitandaoni baada ya kumshauri mmoja wa wafuasi wake aliyetaka mawaidha ya utalii kabla ya kuzuru Kenya kuwa asitumie taulo za Kenya kwani zote zina maradhi ya UKIMWI. Kilichofuta ni msamaha kutoka kutoka Runinga ya CBN anayohubiri mchungaji huyo.

Kando na kusababisha mashirika na viongozi mbali mbali kuomba nsamaha, mtandao huo umetumika pakubwa kuwaunganisha Wakenya hasa wakati wa mashambulio, au wakati wanariadha wanaliwakilisha taifa hili.

Related Topics