Msinione nimekimya - Uhuru aonya

NAIROBI, KENYA,

 

 
'Chaguo langu la atakayenirithi 2022 litawashangaza baadhi yenyu'.
 
Ndio kauli ya hivi punde ya Rais Uhuru Kenyatta ambaye ameonekana kukerwa na viongozi wa kisiasa hususan kutoka eneo la Kati ambao wamekuwa wakimsinikiza kutangaza atakaye muunga mkono wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Badala yake, Uhuru amewakashifu kwa kujihusisha katika siasa zisizokuwa na msingi badala ya kuwahudumia wananchi waliowachagua.
 
Akihutubu mjini Nyeri Rais aidha ameelezea kukerwa na madai ya hivi majuzi wa viongozi hao ambao waliokongamana majuzi mjini Naivasha wakidai kuwa serikali ya Jubilee imelitenga eneo hilo kimaendeleo na wakati uo huo kupuuza dhana za baadhi yao kuwa ushawishi wake kisiasa utakuwa umefifia ifikapo 2022.
 
 
Mapema wiki hii, viongozi hao wa eneo la Kati wakiongozwa na Cecily Mbarire walidai kutengwa kimaendeleo kwa eneo hilo.

Related Topics

Uhuru Kenyatta