×
App Icon
The Standard e-Paper
Informed Minds Prefer The Standard
★★★★ - on Play Store
Download Now

Mtangazaji wa DW Isaac Gamba afariki dunia

NAIROBI, KENYA,
 
Jamaa marafiki na wanahabari kwa jumla waliofanya kazi na mtangazaji wa kimataifa wa lugha ya Kiswahili, Isaac Gamba wanaendelea kuomboleza kifo cha mwanahabari huyo wa Shirika la Deutsche Welle - Swahili.
 
Gamba ameripotiwa kufariki dunia Alhamisi baada ya mwili wake kupatikana chumbani mwake mjini Bonn alikokuwa akiishi. Kwa mujibu wa wanahabari wenza katika shirika hilo, Gamba alikosa kufika kazini kwa siku ya tatu mfululizo hapo jana na kuwalazimu kuripoti kwa polisi walioelekea nyumbani kwake na kumpata ameaga dunia.
 
Aidha, inaarifiwa kuwa Gamba ambaye ni raia wa Tanzania, alijiunga na DW mwaka 2015, amekuwa akilalamikia maumivu ya kichwa kwa muda sasa.
 
Humu nchini Kenya, umahiri wake umedhihirika kufuatia taarifa za kimataifa kutoka DW ambazo hukujia saa saba na saa moja jioni wakati wa Upeo wa Radio Maisha.
Get Full Access for Ksh299/Week
Uncover the stories others won’t tell. Subscribe now for exclusive access
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics

Issac Gamba