×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download App

ERC yatangaza bei mpya ya mafuta

Na Mate Tongola
 
Saa chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Fedha wa 2018 kuwa sheria, Tume ya Kudhibiti Kawi Nchini, ERC imetangaza kupunguzwa kwa bei ya petroli, dizeli na mafuta-taa.
 
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ERC imesema lita moja ya petroli jijini Nairobi itauzwa kwa shilingi 116, dizeli kwa shilingi 108 sawa na lita moja ya mafuta-taa.
 
Jijini Mombasa, lita moja ya petroli itauzwa kwa shilingi 114, kiwango sawa na hicho cha dizeli kikiuzwa kwa shilingi 105 huku lita moja ya mafutaa-taa ikiuzwa kwa shilingi 105.
Wakazi wa Kisumu watanunua lita moja ya petroli kwa shilingi 118, dizeli 109 na mafuta-taa 110.
 
Bei hizo tayari zimeanza kutekelezwa katika baadhi ya vituo vya mafuta nchini.
Get Full Access for Ksh299/Week.
Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics

ERC Fedha