Mswada unaopendekeza kuondolewa ofisini kwa Waziri wa Afya, Sicily Kariuki umewasilishwa bungeni. Jumla ya wabunge mia sabini wametia saini mswada huo uliowasilishwa na Mbunge, Bashir Abdullaih.
Waziri huyo analengwa kutimuliwa kwa kumsimamisha kazi Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, KNH Lily Koros kufuatia kisa ambapo mgonjwa asiyestahili alifanyiwa upasuaji wa ubongo. Waziri huyo anashtumiwa kwa madai ya kukiuka sheria katika kufanya uamuzi huo.