Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Join Thousands Daily
★★★★ - on Play Store
Download App

Hukumu ya kifo ni kinyume na katiba''Mahakama ya Juu yaamua''

Hukumu ya kifo ni kinyume na katiba''Mahakama ya Juu yaamua''
Na Carren Omae
Hukumu ya kifo ni miongoni mwa masuala ambayo watetezi wa haki za binadamu wameifanya kipaumbele humu duniani huku jzao zikiendelea kuzaa matunda  baada ya Kenya kuwa taifa la hivi punde kulegeza kamba kuhusu hukumu hiyo. Huenda kampeni za mashirika mbalimbali kimataifa ya kutetea haki za binadamu kupinga hukumu za kifo, inaendelea kuzaa matunda. 
Japo Mahakama ya Juu Kenya  ilifafanua kwamba haimaanishi kuwa kipengele hicho hakitaondolewa, mahakama hiyo ilisema kwamba kwa mujibu wa katiba kila mkenya ana haki ya kuishi na hivyo kuwapo kwa hukumu ya kifo ya lazima kunakiuka haki hizo. 
Ripoti ya Shirika la Amnesty International TI Mwaka jana ilionesha kuwa licha ya mataifa mengi kuondoa sheria kuhusu hukumu ya kifo, watu wengi wamekuwa wakiuliwa kufuatia maamuzi ya mahakama. Miongoni mwa mataifa 56 duniani ambayo yana sheria ya hukumu ya kifo ishirini na matatu yamekuwa yakiitekeleza kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Mataifa ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini yanaongoza, ambapo zaidi ya watu elfu moja miongoni mwa watu zaidi ya elfu kumi na wanane waliohukumiwa kifo, waliuliwa. Katika utafiti wake TI ilibainisha kuwa asilimia 90 ya visa hivyo vilitekelezwa katika mataifa ya Iran, Iraq, Saudia Arabia na Pakistan.
Aidha hukumu hiyo hutekelezwa nchini Marekani ambapo inaambatana na sheria katika majimbo thelathini na moja. Hata hhivyo katika majimbo kumi na tisa sheria hiyo imeondolewa. Tangu mwaka 1976 ni watu 1,442 ambao wameuliwa kufuatia maamuzi ya mahakama nchini Marekani.
Hayo yakijiri nchini Kenya, mara ya mwisho ambapo hukumu hiyo ilitekelezwa ni  1987. Mwaka 2009 serikali iliwapunguzia hukumu wafungwa wote waliokuwa wamehukumiwa kifo na kuagiza wafungwe maisha.
Francis Muruatetu na Wilson Mwangi, waliohukumiwa kifo miaka kumi na minne iliyopita, waliwasilisha kesi mahakamani kupinga hukumu hiyo kwa misingi kwamba ni kinyume na katiba vilevile inakiuka sheria zingine za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Walipofanya uamuzi majaji, Philomena Mwilu, Jackton Onjwang' na Njoki Ndung'u walikubaliana na walalamishi. Majaji hao waliagiza kwamba kesi dhidi ya wawili hao iwasilishwe katika Mahakama Kuu ambapo watahukumiwa upya.
Uamuzi huo utawasilishwa kwa Spika wa Bunge la Kitaifa ambapo mchakato wa kuifanyia mabadiliko sherria hiyo unatarajiwa kuanza iwapo kutakuwa na haja. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ana kipindi cha miezi minne kuwasilisha ripoti kamili kuhusu hukumu hiyo kwa Mahakama ya Juu.
Je, wazifahamu mbinu zinazotumika kutekeleza hukumu  ya kifo, katika mataifa mbalimbali duniani? Humu nchini, waliohukumiwa kifo walinyongwa. Mataifa mengine ambayo hutumia mbinu ya kuwanyonga wafungwa  ni Botswana, Iran, Sudan, Sudan Kusini, Kuwait na mengine. Nchini Marekani mara ya mwisho mfungwa alinyongwa ilikuwa mwaka 1996.
Mataifa ya Indonesia, Yemen na Somalia hutekeleza hukumu hiyo kwa kuwapiga risasi wafungwa. Aidha taifa la Saudia Arabia ndilo la pekee duniani ambalo hutekeleza hukumu hiyo kwa kuwakata vichwa wafungwa.
Marekani kwa upande wake inatumia mbinu ya kuwadunga aina ya dawa ambayo huwafanya kufariki dunia polepole bila kuhisi uchungu. Hata hivyo  kufuatia kampeni za kupinga hukumu ya kifo, kampuni za kuteneneza dawa zilisitisha mipango ya kuzitengeneza na kuziuza dawa ambazo zilitumika kuwaua wafungwa.
Mbinu hiyo vilevile imewahi kutumika nchini China na Vietnam mwaka 2013.
Vilevile Nchini Marekani mbinu ya kuwapiga na stima wafungwa kwa kutumia kiti maalum ilitumika. Mara ya mwisho kwa mbinu hiyo kutumika ilikuwa mwaka 2013 japo ilipigwa marufuku mwaka 2008.
Kinachosubiriwa kuonwa ni iwapo mataifa 57 yaliyosalia yatafuata mkondo uo huo, na kuiondoa hukumu ya kifo kwani kulingana na sheria kuhusu haki za binadamu za Umoja wa Mataifa za mwaka 1948 sehemu ya nne na ambazo zinatumika hadi sasa, kila binadamu ana haki ya kuishi.


 

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Uncover the stories others won't tell. Subscribe now for exclusive access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics