Na, Beatrice Maganga
Mitihani ya K.C.P.E yang'oa nanga
Matayarisho ya Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane yamekamilika huku mitihani hiyo ikitng'oa nanga rasmi. Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wananchi na wanasiasa kudumisha mazingira bora ili kuwapa watahiniwa fursa ya kufanya mitihani yao bila miingilio. Rais amezungumza wakati wa kukabidhiwa cheti cha ushindi katika marudio ya uchaguzi wa urais.
Akizungumza wakati wa ziara katika shule mbalimbali za msingi, Waziri wa Elimu, Dkt. Fred Matiang'i ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi aidha amewahakikishia watahiniwa kwamba usalama wao umedumishwa na kuwashauri kutokuwa na hofu.
Matiang'i aidha amewashauri watu ambao hawahusiki na mitihani hiyo kutorandaranda kwenye maeneo ya kufanyia mitihani ili kuwapa watahiniwa mazingira yafaayo. Matiang'i aidha amesema watahaniwa watakaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka ujao watakuwa wa kwanza kunufaika na mpango wa elimu bila malipo utakaonzishwa na serikali mwezi Januari. Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini, KNEC, George Magoha aidha amewasihi watahiniwa kujiepusha na udanganyifu, badala yake wajiamini.
Baadhi ya shule ambazo Matiang'i amezizuru akiwa ameandamana na washikadau katika sekta ya elimu vilevile Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinet ni Shule ya Msingi ya Githurai, Shule ya Msingi ya Riruta, Satelite vilevile Shule ya Msingi ya Gatina, Kawangware. Kisa kilishuhudiwa baada ya Matiang'i kuondoka katika shule ya Gatina huku baadhi ya vijana wakianza kurusha mawe kuyaelekeza katika shule hiyo.
Inadaiwa wakazi hao walighaghabishwa na hatua ya Mating'i kutowahutubia, baada ya kuzizuru shule mbalimbali za msingi kutathmini matayarisho ya mitihani wa KCPE utakaong'oa nanga kesho. Ikumbukwe wikendi iliyopita, wafuasi wa mirengo ya NASA na Chama cha Jubilee walikabiliana eneo hilo hali iliyochangia uharibifu wa mali.?