MTALII AFARIKI MLIMA KENYAMTALII AFARIKI MLIMA KENYA

MTALII AFARIKI MLIMA KENYA
MIKE NYAGUOKA
Shirika la Huduma za Wanyamapori, KWS linatafuta mbinu ya kuondoa mwili wa mtalii mwenye asili ya kichina aliyeaga dunia baada ya kukwea Mlima Kenya. Mtalii huyo aliaga dunia jana saa tisa usiku baada ya kukwea hadi eneo la Batiana ambalo ndilo miongoni mwa maeneo yaliyo juu zaidi.
Kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la Uhifadhi Wanyama-pori, Ngugi Gecaga, mtalii huyo aliteleleza na kuangukia jiwe.
Huenda ikachukua hadi siku tatu kuondoa mwili huo kufuatia hali mbali ya anga katika mlima huo.

Related Topics