Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Mataifa ya Kenya na Somalia yameafikiana kurejelea safari za moja kwa moja za ndege kati ya Nairobi na Mogadishu pamoja na kufunguliwa kwa vituo viwili ambavyo vitatumiwa na wanaoingia na kutoka mataifa haya mawili.