Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download App

Mark Bor akana kulikuwa na makubaliano kuhusu mkataba wa madaktari

Na, Mike Nyagwoka

Huku mgomo wa madaktari ukiingia siku ya 80 mikakati ya kusitisha mgomo wa madaktari huenda ikatatizwa zaidi  kufuatia hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mark Bor kukana kuwapo kwa mkataba rasmi baina ya madaktari na serikali Hayao yanajir huku Waziri wa Fedha, Henry Rotich akisema iwajabikia tu miakataba ya wahudumu wa faya iliyotiwa saini kati ya Januari na Juni mwaka 2013 hivyo basi kuashiria kuwa vilevile itawajibikia mktaba wa madaktari uliotiwa saini Juni mwaka 2013.
Katika vikao baina ya Kamati za Afya na Leba na Chama cha Madaktari, KMPDU bungeni, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mark Bor amekuwa na wakati mgumu kujibu maswali kuhusu jinsi alivyohusika katika kubuni mkataba ambao umezua utata. Bor hasa ametakiwa kueleza suala la ni kwa nini aliutia saini mkataba huo licha ya kwamba alikuwa ameondolewa katika wadhifa wa Katibu Mkuu.
Hata hivyo akijitetea, Bor amesisitiza kuwa stakabadhi alizotia saini hazikuwa mkataba rasmi bali nakala za maafikiano ya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na kwamba mkataba huo ungesainiwa rasmi baadaye. Hata hivyo kauli ya Bor haikuwafurahisha wabunge ambao wamemtaka kuifafanua kauli yake.
Kwa upande wao, madaktari wamesisitiza kwamba mkataba rasmi ndio uliostahili kusajiliwa na mahakama chini ya kipindi cha siku 14. Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa KMPDU, Mwachomba Chibanzi kuchelewa kusainiwa kwa mkataba ndio sababu kuu ya wao kwenda mahakamani ambapo walipata agizo la kuishurutisha serikali kuuidhinisha mkataba huo.
Ikumbukwe madaktari walitangaza mgomo pende  Tume ya Kuratibu Mishahara SRC ilipoweka wazi ripoti ya tathmini ya wafanyakazi wote wa umma - ikisema haikuwa imependekeza nyongeza yoyote kwa mujibu wa mkataba wa mwaka 2013. Hata hivyo Afisa Mkuu Mtendaji wa SRC, Sarah Serem ambaye vilevile amefika mbele ya kamati hizo leo amepinga madai hayo akisema tathmini hiyo iliambatana na mapendekezo ya mishahara inayofaa kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka huu. Mazungumzo ya kusuluhisha mgomo huo yanatarajiwa kuendelea.

 

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Fact-first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Follow The Standard on Google News

Related Topics