Madaktari waapa kuendelea kugoma

Na, Rosa Agutu

Viongozi wa muungano wa Madaktari nchini KMPDU wamefanya mkutano leo jijini Nairobi na kusisitiza kwamba mgomo wao ungalipo. Madakatari hao wamesisitiza kwamba mkataba wa malipo waliotia saini mnamo mwaka 2013 ni halali na ni sharti utekelezwe.
Mwenyekiti wa Muungano huo Samwel Oroko, amesema mkataba huo si wa nyongeza ya mishahara pekee kwani pia unahusu kuongezwa kwa idadi ya madaktari, kupunguzwa kwa saa sa kufanya kazi kutoka saa 168 kwa wiki hadi saa 40 kwa wiki.
Katibu Mkuu wa muungano huo, Ouma Oluga  kwa upande wake  amesema hakuna mazungumzo yatakayoendelea hadi wakuu wa madaktari watakapo maliza kifungo chao cha mwezi mmoja. Ikukumbukwe wiki mbili zilizopita mahakama ilitoa amri yakukamatwa na kufungwa kwa viongozi hao iwapo mgomo hautasitishwa ifikapo ilhamisi wiki hii.  

 

Related Topics